Posts

MAPENZI NA USHIRIKINA

Image
kUNA Mambo makuu mawili yanayo wafanya wapenzi kuendeana kwa waganga, nayo ni: 1. KUTOJIAMINI BINAFSI YAKE. 2. WOGA NA WASIWASI WA KUACHWA. Ukihisi mpenzi wako anakuendea kwa waganga, huyo achana nae, maana mtu ambaye alikupata kwa kauli na mkakubaliana kuwa wawili halafu baadaye anahisi upendo unaompenda nao hautoshi akitaka uzidishe zaidi ya hapo na wakati huo huo yeye binafsi hasimamii kukuongezea upendo ambao utalivusha pendo lenu kwenda kwenye PENDO JIPYA hakika huyo atakupa mikosi na sio jingine. Mapenzi ni UBUNIFU wala sio uchawi, Moyo haulogwi mazeee... Uchawi mzuri wa moyo ROGA kizungu MAHABA BATANIIII!, hapo hata shetani atakiri ya kuwa MUNGU mkubwa. Nikwambie tuu kwamba, ulimi laini ni suruhisho la MAPENZI... Huna haja ya kubebeshwa mizigo wakati siraha uko nayo ni vile hujui na hutaki kujuwa. Yapambe mahusiano/Ndoa yako kwa kujituma na kuwa mwingi wa ubunifu uone kama kuna haja ya kuogopa ama kuhisi wasiwasi kwenye Mapenzi yako.  Kama unaamini muunganiko wako

KINACHOTESA KWENYE MAPENZI

Image
Kinachotesa kwenye MAPENZI ni MATARAJIO na MTAZAMO wa PENZI husiaka, kuacha ni ngumu lakini ukithubutu ni USHINDI, kuachwa ni hatari lakini ukiipokea hali hiyo ni TIBA ya STRESS na yote hayo yanahitajiana kulingana na vile ambavyo unapenda kuishi na FURAHA yako MWENYEWE.  Na usijaribu kumshika mtu ambaye yeye Mwenyewe amepanga akuondoke, akitaka kuondoka mwache aende maana ukimzuia na hana mpango nawe ITAKUGHARIMU. Je, unalijuwa donda ndugu la MAPENZI?, Donda la mapenzi ni MAZOEA.  Unajuwa kupenda kila mmoja anapenda vizuri tu, Lakini ili uweze kudhihilisha pendo lako la ndani ni pale unapokuwa UMEMZOEA MTU HUYO, kama hujamzoea Mpenzi wako ni ngumu sana kuumia akiondoka, wanaoumia juu ya Mapenzi ni wale ambao kwa hakika WAMEMZOEA MTU kiasi kwamba hakuna siku ilokwenda bila kukutana, kuongea na kutumiana jumbe za mahaba.  Kwa maana hiyo ukitaka uishi salama kwenye mapenzi achana na kumzoea mtu wako, mazoea yanatesa hasa ukijitazama na kukumbuka zile nyakati ambazo Mwenza wa

UNACHOHITAJI KWENYE MAPENZI

Image
Usimfikirie mtu ambae hana mda hata kidogo wa kukufikiria wewe.. usipoteze nguvu zaidi kwa mtu ambae hata hajibu ujumbe wako kulingana na vile ulivyohitaji aseme, unapoteza hisia zako na mda wako kwa mtu ambae haoni thamani yako.  Upendo ni kitu ambacho hakilazimishwi, Inaweza kutokea au isotokee na kama ikitokea inatokea kwenye mkonyezo wa jicho ama ishara ya vidole.  Upendo si kitu unachoweza kuomba au kuulizia mara kwa mara ila ni kitu ambacho kinagusa uwajibikaji, kwaiyo kama mtu hawezi kurudisha upendo usimpe umuhimu kwenye maisha yako. Usipoteze mguso wako kwa watu wasiothamini pendo lako... kwa yule ambae kuwepo kwako au kutokuwepo hakujalishi na anakuchukulia kama mtu wa kawaida tu.  Usichukie watu ambao walikuhitaji pindi walipotaka kitu kutoka kwako maana hao ndiyo watakaokujenga kujitambuwa kwamba wewe ni wa muhimu pia. Kwaiyo usitoe hisia zako au mda kwa mtu ambae hata hazihitaji na kama anazihitaji ni kwa MASRAHI yake na sio kujenga muunganiko wa hisia zenu.  

USITAFUTE MWENZA, TAFUTA MWENZA SAHIHI

Image
Sio kila Mwanaume anaweza kumsababisha Mwanamke awe na nuru na muonekano mzuri, vivohivyo sio kila Mwanamke anaweza kumsababisha mwanaume awe na nuru pamoja na muonekano mzuri, maana katika UPENDO kuna uhitaji wa NAFSI na hapo ndipo paliposababisha wawili KUHITAJIANA. Hakuna kazi ngumu kwenye maisha ya Mapenzi kama MTU kumpa MWENZA wake FURAHA. Wengi huishi kwenye mahusiano ama ndoa kwa mazoea na kutunza heshima kwenye jamii huku mioyo yao imejaa madonda ambayo hayawezi kuponywa wala kutibiwa maana aliyesabisha hajui kama ameumiza moyo wa mwenza wake, Kukosea sio kosa maana ni kujisahihisha, kosa ni kurudia kosa kwa sababu ni makusudi kutokana na ukweli kwamba MTU ALIISHA AMBIWA AMA KUONYWA lakini bado anarudia kosa lile lile. Mtu asiyejuwa kutuliza MOYO wa mwenza wake huyo hajajipanga kumpa mwenza wake FURAHA. Huwezi kusema niko kwenye Mahusiano ama ndoa wakati ndani ya moyo wako umejawa huzuni na simanzi pamoja na woga ulojawa kukata tamaaa.  Usiishi maisha ya MAPENZI kwa

PAPASO LA LEO

Image
1. Kukaa mbali na mke kwa muda mfupi inaweza kuimarisha mafungamano ya ndoa yenu, lakini kukaa mbali kwa muda mrefu inaweza kugeuka nyenzo ya kuibomoa. 2. Yafahamu maumbile ya mwanamke ili uweze kujua njia sahihi ya kushughulika naye bila kutumia maguvu na misimamo mikali. 3. Usiruhusu mgogoro wenu uendelee mpaka siku ya pili. 4. Epuka kuzungumzia mambo ya zamani yanayohusu mwanamke mwingine, iwe mchumba au mkeo wa zamani. 5. Epuka kuigiza, ishi maisha yako halisi, usitarajie miujiza. 6. Muoneshe mkeo jinsi unavyompenda kila unapopata fursa. 7. Usikubali kusalimu amri mbele ya msongo na wasiwasi. Daima upambe wajihi wako kwa tabasamu, ukunjufu na uwe mwenye matumaini. 8. Epuka kumponda mwenzako kwa kila dogo na kubwa. 9. Siku zote uweke mzozo wenu katika wigo mdogo, usijaribu kuupanua. Lidhibiti tatizo kabla halijakuponyoka. 10. Wivu, shaka na tuhuma ni maadui wa ndoa yako. Shughulika na uhalisia, usishughulike na dhana na mambo ya kufikirika

ISHI NA MWENZA WAKO KULINGANA NA KIPATO CHENU

Image
Nikazi ya MWANAMKE kutaka vitu vya gharama lakini ni kazi yako kuhakikisha mnaishi kutokana na kipato chenu. Kanuni ya kwanza kabisa katika ndoa yako baada ya kumpenda mke wako, mwanaume unapaswa kuishi kutokana na kipato chako, narudia unapaswa kuishi kutokana na kipato chako, Najua na ni kazi ya mwanamke kutaka vitu vya gharama, kutaka vitu ambavyo mashoga zake wananunuliwa lakini kamwe usimpe mkeo kitu ambacho huna uwezo nacho, hapa nikimaanisha usikope na wala usijinyime ili kumpa vitu kwaajili ya kushindana na marafiki zake. Kopa kwa ugonjwa, chakula na shida nyingine lakini si kwaaajili ya kumfurahisha mwanamke. Kwanza hatafurahi kama anashindana, lakini pili atakuchoka mapema pale ambapo utamzoesha aina flani ya maisha na kushindwa kumpa huko mbeleni. Hata kama ndugu zake wana pesa na uwezo mkubwa kamwe usikubali wakusaidie kutunza familia yako, Kwamba anunue gauni nzuri au alipie mchango wa Kichen Party kutoka kwa hela ya Mama yake. Kama siku mkeo akikuomba pesa ya ku

UMUHIMU WA KUJIANDAA NA MAISHA YA NDOA

Image
Katika kumuumba kwake mwanadamu, Mwenyezi Mungu aliweka utaratibu wa kuwepo mahusiano kati ya mume na mke, ili kuendeleza uzao kwa wanadamu, kuwaondolea upweke na kuwatunukia utulivu, faraja, huruma, mapenzi, upendo na ushirikiano. “Na katika ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo ishara kwa watu wanaofikiri”. Arruum21. Kutokana na Mwenyezi Mungu kuwajengea wanadamu mahusiano hayo ya jinsia mbili tofauti, aliweka sharti na utaratibu wa mahusiano hayo, nao ni utaratibu wa ndoa kati yao. Kimsingi ndoa kwa wanadamu ni uhalalishaji adilifu wa mahusiano ya mume na mke. Mahusiano ambayo yamewekewa utaratibu mahususi ya kukubalika nakutambulika rasmi. Kusudio la kuwepo utaratibu huu wa ndoa ni kuweka mipaka ya kimahusiano miongoni mwa wanadamu na kuondoa vurugu za watu kuingiliana hovyo. Hii ina maana ya kudhihirisha kwamba mke au Mume wa mtu anah