ISHI NA MWENZA WAKO KULINGANA NA KIPATO CHENU

Nikazi ya MWANAMKE kutaka vitu vya gharama lakini ni kazi yako kuhakikisha mnaishi kutokana na kipato chenu.

Kanuni ya kwanza kabisa katika ndoa yako baada ya kumpenda mke wako, mwanaume unapaswa kuishi kutokana na kipato chako, narudia unapaswa kuishi kutokana na kipato chako,
Najua na ni kazi ya mwanamke kutaka vitu vya gharama, kutaka vitu ambavyo mashoga zake wananunuliwa lakini kamwe usimpe mkeo kitu ambacho huna uwezo nacho, hapa nikimaanisha usikope na wala usijinyime ili kumpa vitu kwaajili ya kushindana na marafiki zake.

Kopa kwa ugonjwa, chakula na shida nyingine lakini si kwaaajili ya kumfurahisha mwanamke. Kwanza hatafurahi kama anashindana, lakini pili atakuchoka mapema pale ambapo utamzoesha aina flani ya maisha na kushindwa kumpa huko mbeleni.
Hata kama ndugu zake wana pesa na uwezo mkubwa kamwe usikubali wakusaidie kutunza familia yako, Kwamba anunue gauni nzuri au alipie mchango wa Kichen Party kutoka kwa hela ya Mama yake.

Kama siku mkeo akikuomba pesa ya kununulia kitu cha starehe, tuseme gauni jipya na ukamuambia huna au unayo lakini ukamuambia tufanye kitu flani kwanza akarudi na kukuambia Mama kaninunulia, basi chukua kiberiti na lichome moto muambie wewe ndiyo mwanaume na huwezi kuhudumiwa na Mama yake. Siku nyingine akirudia kitu kilekile, mchukue nenda mbele ya Mama yake na lichome moto hilo gauni?

Iko hivi sasa hivi utaona raha kwakua ni Mama yake kamnunulia, kwakua ni Kaka yake kamnunulia lakini ipo siku Mama yake hatakua nacho, Kaka yake hatakua nacho au watakua mwamemchoka tu na hawatampa, atahitaji kama huna basi atatafuta mwanaume wa kumhudumia. Nilazima mkeo ajue kuwa mtaishi kutokana na uwezo wenu na kama hawezi kuishi hivyo muambie basi kwa heri.

Nilazima uamue kuwa mwanaume ndani ya nyumba, lakini hapa nataka mnielewe, sio kama mwanamke anayetaka vitu vizuri ni mbaya au ni shetani, hapana wanawake wameumbwa hivyo kutaka vitu vizuri hivyo ni kazi yako wewe mwanaume kumdhibiti asivuke mipaka kwani akivuka mipaka atapata uteja wa vitu vizuri mpaka itafikia hawezi kujizuia tena na akichepuka kosa halitakua lake bali lako!

Sasa kuna swali ambalo linakuja kichwani, je vipi kama mwanamke ana pesa zake, ana kazi yake nzuri je akihitaji vitu vizuri nitafanyaje? Kama ana pesa zake ni sawa kujinunulia viztu vizri huwezi kumkatasa lakini usimpe uhuru wa kufanya kitu bila kukuambia na bvila kupaata maelezo ya uhakika. Anapesa kweli, ni zake lakini haimaanishi kuwa huwezi kumpangia na pia haimaanishi kuwa hataki umpangie!

Hii ni mada pana lakini iko hivi kila mwanamke apende asipende anapoolewa kuna uhuru amabo hata yeye mwenyewe hautaki kwani akiupata atajihisi kama kajioa na nilazima atafute mwanaume wa kumsimamia na kama si wewe mume wake basi atakua mwingine! Sasa kuna vitu na vitu ambavyo unaweza kumpa uhuru mwanamke kununua au kufanya bila kujadiliana na wewe lakini kuna vingine nilazima mjadiliane hata kama hela ni ya kwake.

Vitu kama nguo, nywele, viatu na makorokocho mengine anaweza kununua, lakini vitu kama Gari, kujenga na vingine vikubwa nilazima mjadiliane. Narudia mjadiliane na muelewane na si umkataze kuvifanya. Mwanamke unaweza sema ni hela yangu lakini kama hautajadiliana na mume wako basi jua ni kama unavunja ndoa yako, lakini kujadiliana huku kusiwe kwa upande mmoja.

Kwamba wewe mwanaume unanunua Gari hata humuambii mkeo, unajenga mkeo hajui halafu uantaka yeye akifanya hivyo akuambie. Hapana Dada yangu kama uko kwenye ndoa ya namna hiyo basi nawewe fanya yako, ila kama mwanaume anakuambia mambo yake ni muwazi na wewe unapaswa kuwa muwazi hata kama hela ni zako hivyo na wewe mwanaume kama unataka uwazi nilazima uwe muwazi na si kila mmoja kumzunguka mwenzake.

Comments

Popular posts from this blog

MWANAUME MWENYE MALENGO NA WEWE UTAMTAMBUA KWA HAYA

MAPENZI NA USHIRIKINA

UMUHIMU WA KUJIANDAA NA MAISHA YA NDOA