PAPASO LA LEO

1. Kukaa mbali na mke kwa muda mfupi inaweza kuimarisha mafungamano ya ndoa yenu, lakini kukaa mbali kwa muda mrefu inaweza kugeuka nyenzo ya kuibomoa.

2. Yafahamu maumbile ya mwanamke ili uweze kujua njia sahihi ya kushughulika naye bila kutumia maguvu na misimamo mikali.

3. Usiruhusu mgogoro wenu uendelee mpaka siku ya pili.

4. Epuka kuzungumzia mambo ya zamani yanayohusu mwanamke mwingine, iwe mchumba au mkeo wa zamani.

5. Epuka kuigiza, ishi maisha yako halisi, usitarajie miujiza.

6. Muoneshe mkeo jinsi unavyompenda kila unapopata fursa.

7. Usikubali kusalimu amri mbele ya msongo na wasiwasi. Daima upambe wajihi wako kwa tabasamu, ukunjufu na uwe mwenye matumaini.

8. Epuka kumponda mwenzako kwa kila dogo na kubwa.

9. Siku zote uweke mzozo wenu katika wigo mdogo, usijaribu kuupanua. Lidhibiti tatizo kabla halijakuponyoka.

10. Wivu, shaka na tuhuma ni maadui wa ndoa yako. Shughulika na uhalisia, usishughulike na dhana na mambo ya kufikirika

Comments

Popular posts from this blog

MWANAUME MWENYE MALENGO NA WEWE UTAMTAMBUA KWA HAYA

MAPENZI NA USHIRIKINA

UMUHIMU WA KUJIANDAA NA MAISHA YA NDOA